Monday 26 September 2011

kuweni makini mnao nunua nyumba au viwanja!!!

View Post Tangazo hili halina tofauti yo yote na yale tunayoyasoma katika "Sell & Buy", "Advertise DAR" au booklets zingine zinazotangaza biashara. Watanzania inabidi tuwe wabunifu wa "kuonyesha na kuiuza expertise" yetu tuliyonayo kwa kina zaidi na bayana. Maelezo hayo yoote yangetosheleza iwapo ExpertBroker angeandika ktk website yake yenye picha, maelezo ya nyumba/viwanja, locations, bei zake na contacts (simu/email).

Pia umefikia wakati muafaka wa Estate/Property owners and Agents KUJENGA NYUMBA kisha kuziuza ama kuzipangisha/kuziuza (purchase-tenant schemes) kama vile yanavyofanya makampuni/mashirika ya Kenya (HFCK, Nairobi City Council, n.k.). Ununuzi wa viwanja, kupata hati na usimamizi wa ujenzi hapa Nchini ni usumbufu mkubwa na umejaa ufisadi kiasi cha kukatisha tamaa sisi wajenzi wadogo. Hebu jaribu kubadili tangazo lako na utupatie "mtandao wenye hadhi ya kitaalam" pamoja na templates za application forms, etc. ili tunaohitaji viwanja/nyumba tuanze kuchangamkia mara moja

No comments: