Katika uhusiano wa kimapenzi ni vyema sana kuwa makini kwani kuna mambo ambayo yanaweza kutokea na hivyo kufanya mapenzi kuwa machungu. Mfano mkubwa ni migogoro ambayo inasababishwa na kukosekana uaminifu ambapo kwa namna moja au nyingine hupelekea wapenzi kugombana. kumekuwa na matukio mbalimbali ya ugomvi baina ya wapendanao ambapo hutokana na kushindwa kutafuta suhuhu ya matatizo kwa njia nzuri iliyo sahihi bila madhara na hivyo hujikuta wakiishia pabaya, Wengine hufikia hatua ya kupigana, kunywa sumu, kuua na hata kutengana. Ukweli ni kwamba ni vyema kuwa makini inapotokea migogoro kwani inaweza kuleta balaa kubwa zaidi.
Wawili wapendanao inapotokea kuna ugomvi basi ni vyema kukaa chini na kuzungumza bila ya kukwaruzana kwani kupiga ama kupigana haisaidii chochote bali huongeza tatizo jifunze kuwa mpole kuepuka hasira ambazo zinaweza kuwa hasara katika maisha yako MAPENZI YANAWEZA KUYAGEUZA MAISHA KUWA MACHUNGU kwa mnao taka kununua vitabu ingia humu http://www.adeladallykavishe.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment