Wednesday, 18 April 2012

MAMA NA MWANA IN STYLE



iyo miwani na top dress uwiiii nimependa je, this is how women should dress in style; she's so happy eeeh! see her kucha utapenda tu usipopenda basi ww utakuwa na wivu!

Monday, 16 April 2012

Mapenzi yanaweza kuyafanya maisha yakawa mafupi na machungu



Katika uhusiano wa kimapenzi ni vyema sana kuwa makini kwani kuna mambo ambayo yanaweza kutokea na hivyo kufanya mapenzi kuwa machungu. Mfano mkubwa ni migogoro ambayo inasababishwa na kukosekana uaminifu ambapo kwa namna moja au nyingine hupelekea wapenzi kugombana. kumekuwa na matukio mbalimbali ya ugomvi baina ya wapendanao ambapo hutokana na kushindwa kutafuta suhuhu ya matatizo kwa njia nzuri iliyo sahihi bila madhara na hivyo hujikuta wakiishia pabaya, Wengine hufikia hatua ya kupigana, kunywa sumu, kuua na hata kutengana. Ukweli ni kwamba ni vyema kuwa makini inapotokea migogoro kwani inaweza kuleta balaa kubwa zaidi.





Wawili wapendanao inapotokea kuna ugomvi basi ni vyema kukaa chini na kuzungumza bila ya kukwaruzana kwani kupiga ama kupigana haisaidii chochote bali huongeza tatizo jifunze kuwa mpole kuepuka hasira ambazo zinaweza kuwa hasara katika maisha yako MAPENZI YANAWEZA KUYAGEUZA MAISHA KUWA MACHUNGU kwa mnao taka kununua vitabu ingia humu  http://www.adeladallykavishe.blogspot.com/

Thursday, 12 April 2012

LULU AFIKISHWA MAHAKAMANI..

Muigizaji wa Filamu nchini anaehusishwa na kifo cha Muigizaji Mwenzie,Marehemu Steven Kanumba,Bi Elizabeth Michael a.k.a Lulu amepandishwa kizimbani mapema leo asubuhi kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam kwa kusomewa mashtaka yake kuhusiana na kuhusika kwa kifo cha Muigizaji huyo nguli hapa nchini.

Elizabeth Michael amesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu Agustino Mmbando na wakili Elizabeth Kaganda ya mauaji ya Muigizaji wa Filamu nchini,Marehemu Steven Kanumba yaliyotokea huko sinza vatcan jijini Dar es Salaam april 7 mwaka huu.

Elizabeth Hakutakiwa kujibu chochote Mahakamani hapo kwani mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji. Kesi hiyo imeahirishwa na kupangwa kusikilizwa tena april 23 mwaka huu. Muigizaji huyo aliletwa mahakamani hapo kwa mwendo wa kasi kama mshale na kwa ulinzi mkali na pia ndivyo alivyoondolewa Mahakamani hapo Kwa gari ndogo nyeupe aina ya suzuki grand vitara yenye nambari za usajiri T 848 BNV huku kwenye kioo nambari zake zikisomeka PT 2565.

BBC SWAHILI HAD THIS TO SAY;

Amefikishwa mahakamani ikiwa ni siku nne, tangu alipokamatwa mara baada ya kifo cha msanii huyo ambaye inaaminika kuwa walikuwa na uhusiano wa Kimapenzi.
Taarifa zinazohusiana
Afrika, Tanzania
Mbele ya Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam,Bi Augustina Mbando,Elizabeth Michael Kimemeta ajulikanaye kama Lulu kwa jina la Usanii,aliwasili mahakamani hapo akiwa chini ya Ulinzi mkali wa askari Polisi waliokuwa wamevaa kiraia na wengine wakiwa wamejihami kwa silaha.
Mara baada ya Kufikishwa mahakamani,upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa serikali Bi Elizabeth Kaganda ulimsomea shtaka moja ambalo ni la mauaji, kosa ambalo ni kinyume cha sheria ya kanuni ya adhabu kifungu cha 196.

Wakili huyo wa serikali Bi Elizabeth Kaganda,alidai mbele ya mahakama kuwa mnamo tarehe 07 mwezi April mwaka 2012,katika eneo la Sinza Vatican,msanii Elizabeth alimuua msanii Steven Kanumba.

Akiwa amevalia gauni kubwa lijulikanalo kama dera lenye rangi ya Njano mtandio wa rangi ya waridi na kandambili nyekundu mshtakiwa alionekana kutokuwa na wasi wasi pamoja uzito wa tuhuma za mauaji anayokabiliwa nayo huku akijibu maswali kadhaa kuhusu wasifu wake.
Msanii huyo alikanusha kuwa na umri wa miaka 18 baada ya kuulizwa ,ambapo yeye amesisitiza kuwa ana umri wa miaka 17, hii ikiwa ni tofauti na habari ambazo zimekuwa zikiripotiwa kuhusu umri wa msanii huyo ambaye sasa anatambulika kama mshtakiwa.
Kesi hii ya mauaji inatajwa kwa mara ya kwanza na mshtakiwa hakutakiwa kukiri wala kukana mashtaka.
Upande wa mashtaka umeieleza mahakama kuwa kesi bado iko kwenye upelelezi ambapo inatarajiwa kutajwa tena April 23 mwaka huu.
Mshtakiwa amepelekwa rumande hadi siku hiyo wakati kesi hii itakapotajwa tena.
Kwa upande mwingine tukio la kufikishwa mahakamani kwa mtuhumiwa huyo kumefanywa kwa usiri mkubwa na kufanya waandishi wa habari wengi wameshindwa kufuatilia kwa karibu tukio lenyewe.
Kufikishwa mahakamani kwa msanii huyo na kusomewa shtaka la mauaji ya Kanumba kumetokea siku moja baada na Marehemu Steven Kanumba kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni.
Mazishi yake yalichukua sura ya kitaifa kutokana na umaarufu aliojijengea msani huyo katika jamii ya watanzania na hata nchi za nje

MAZISHI YA KANUMBA YALIKUWA HIVI..








 watu walikuwa wengi sana, sijawahi ona




 hawa watoto wameingiza sana na kanumba

baada ya kumuaga hivi ndivyo palivyo baki, mungu amlaze maali pema peponi ameni

Tuesday, 10 April 2012

TUTAKUKUMBUKA DAIMA...




 mama salma kikwete
 mama yake kanumba akilia, inauma sana
 mama wa kanumba na mama salma kikwete
muheshimiwa nae alikuwepo akiweka saini

POLISI BADO WAKIFATILIA NI NINI CHAZO CHA KANUMBA KUFARIKI.. HIVI NDIVYO WANAVYO SEMA....



RPC wa Kinondoni-Charles Kenyela said kwamba POMBE kali (Whisky) aina ya Jacky Daniel, imetajwa kama chanzo cha kifo cha mwigizaji nyota wa filamu nchini, Steven Charles Kanumba aliyefariki usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake, Sinza, Dar es Salaam.


ACP Charles Kenyela amesema leo kwamba uchunguzi wa awali unaonyesha hivyo, lakini bado wanaendelea na uchunguzi zaidi, ili kujua zaidi.

ACP Kenyela amesema kwamba Kanumba wamefanikiwa kumuhoji mtuhumiwa wa kwanza katika tukio hilo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na katika maelelezo yake amekanusha kumsukuma Kanumba.


Vyombovingi vya habari vilimnukuu ndugu wa Kanumba, Sethi jana akisema kwambaLulu alimsukuma mwigizaji mwenzake huyo katika ugomvi wao wa wivu wa kimapenzi hadi akaanguka na Akizungumzakutokana na maelezo ya Lulu, Kamanda huyo alisema kwamba; ugomvi wao ulitokana na Kanumba kutaka kumdhibiti Lulu wakati akizungumza na simu.
“Kanumbaaliamua kumfuata Lulu nje huku akifoka kwa sauti, akitaka aelezwe kwa nini alitoka nje kupokea simu, huku akimtuhumu kuwa huenda alikuwa akizungumza na mwanaume mwingine.


Baadaya Lulu kuona Kanumba anamfuata, aliamua kukimbia kutoka nje ya geti, lakini kabla hajafanikiwa kufungua geti, Kanumba alimkamata na kumrudishwa ndani. Kanumba akiwa amemshikilia, waliingia wote chumbani na kufunga mlango. Sasa haijulikani nani aliyefunga mlango, ingawa maelezo ya Lulu, anadai kuwa aliyefunga mlango ni Kanumba,”


Akiendeleakumnukuu Lulu, Kamanda huyo anasema; “Baada ya Kanumba kufunga mlango, alimuona akilegea na kujigonga kisogo chake kwenye ukuta wa chumba hichokabla ya kuanguka chini,”alisema.
Alisema uchunguzi wa tukio zima ukikamilika, hatua inayofuata ni kumpeleka Lulu mahakamani kama mtuhumiwa wa mauaji.


Saturday, 7 April 2012

JAMANI! KANUMBA AMEFARIKI JANA USIKU

 mdogo wake kanumba akiojiwa nini chazo cha kifo cha marehemu, jamani inasikitisha sana!
 picha ya marehemu

 inasemekana chazo ni huyu lulu, alienda kwa kanumba wakapanga watoke out basi kanumba akaingia kuoga akajiandaa; akatoka chumbani akamkuta lulu anaongea na simu na mwanaume mwingine basi ugomvi ukanzia hapo! lulu akamsukuma kanumba akapigiza kisogo aka dondoka chini lulu akaenda kuita darkitari. kwa sasa lulu yuko polisi osterbay kwa ajili ya maojiano na polisi.
 jamani watu wanazimia kama mnavyo ona hapa

Tuesday, 3 April 2012